Je utajuaje kama uzito wako upo sawa au umepitiliza.

🍃⚪*_ JINSI YA KUJUA KAMA UNA UZITO WA WASTANI,UZITO ULIOPITILIZA AU UZITO WA CHINI_*
Na Dr jimmy 0620165254

 🍃⚪ Watu wengi wana uzito uliokithiri na wengine wana uzito wa chini kupita kawaida bila ya wao wenyewe kujua na yote haya ni hatar kwa Afya yaani uzito ukizid ni hatar na uzito ukiwa chini zaidi ni hatar pia kiafya hivyo mtu anatakiwa awe na uzito wa wastani ( normal weight).

 🍃⚪ Ili kujua kama una uzito unaostahili Uwiano kati ya Kilo (Kg) na urefu katika mita za mraba hutumika kujua

*_ 🍃⚪ BODY MASS INDEX (BMI)_*:
Ni uwiano kati ya Uzito wa Mwili katika kilogramu (Kg) na kimo chako katika Mita za Mraba (Meters Square).Hivyo kizio(SI UNIT) ya Body mass Index ni *Kg/m²*.

 🍃⚪ Hivyo mtu akitaka kujua kama uzito wake upo sawa ama hauko sawa kiafya atapima uzito wake kisha atagawa kwa kimo chako kwenye mita za Mraba.

*Mfano*
Umefanya vipimo ukajikuta na

Uzito(Kilo)= 65 kg
Kimo(Cm)= 180 cm=1.8 m.

Kutafuta BMI
Formula,

BMI= Uzito(Kg)÷Kimo(m²)
        
   =65 kg ÷ 1.8²
   =20.06 ~20.1
BMI = *20.1 kg/m²*

*Kwahyo BODY MASS INDEX(BMI)= 20.1kg/m²*

▶️Ukifanya Calculations ukapata BMI basi unatakiwa ulinganishe katika BMI zifuatazo ili ujue kama uzito wako uko sawa,umezdi ama upo chini ya uzito wa kawaida:⤵️⤵️

1⃣ Chini ya 18.5 kg/m²
_CHINI YA UZITO UNAOTAKIWA (Underweight).

2⃣ Kuanzia 18.5 hadi 24.9 Kg/m²
_UZITO UNAOSTAHILI(normal weight

3⃣ Kuanzia 25-29.9 kg/m²
_UZITO ULIOZIDI KIASI (Overweight)

4⃣ Kuanzia 30 kg/m² na zaid.
_KITAMBI(obesity)

_BMI classification. Global Database on Body Mass Index.World Health Organization.2006

_Madhara yanayotokana na kuzid kwa uzito(overweight)_

Kutokana na vituo kwaajili ya kudhibiti na kujikinga na Magonjwa, centers for Diseases Control and Prevention(CDC),yafuatayo ni madhara ya kuzidi kwa uzito wa Mwili:

▶️ Presha ya kupanda (Hypertension)
▶️ Kuzidi kwa Lehemu (Cholesterol) mwilini
▶️ Kisukari (type ll diabetes)
▶️ Magonjwa ya mfuko wa nyongo(gallbladder diseases)
▶️ Matatizo ya joints(Osteoarthritis)
▶️ Matatizo ya upumuaji
▶️ Saratani(Cancer) kama vile saratani ya utumbo,matiti,figo, ini nk
▶️ Nk.

*_Hatari ya kuwa na uzito wa chini kuliko kawaida(Underweight)_*

▶️ Utapia mlo
▶️ Anemia
▶️ Matatizo ya mifupa(Osteoporosis)
▶️ Kushuka kwa kinga ya mwili
▶️ Kudumaa
▶️ Kutokwa mimba kwa wanawake(Miscarriage) hasa katika miezi mitatu ya mwanzo(first trimester)
▶️ Nk.

*_Hivyo basi hakikisha una uzito wa kawaida usizid wala usipungue_*

Kwa wale ambao wana uzito uliopitiliza wanaweza kufanya mazoezi na kuweka sawa Milo yao na uzito ukarudi sawa ama kwa wale ambao ni wavivu wa kufanya mazoezi kutokana na sababu mbali mbali basi ipo dawa  inauwezo mkubwa wa kupunguza uzito na kukufanya urudi katika hali ya kawaida.

Kwa wale ambao uzito wao upo chini zaidi ya kawaida basi wajitahid kula mlo kamili ili waweze kuepukana na matatzo ambayo yanaweza kuwapata kutokana na kuwa na uzito wa chini zaidi ya inavyotakikana.

Kwa wale ambao uzito wao upo sawa basi wajitahidi kuhakikisha 

Health 
Tunajali afya yako


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi mmea huu inavyotibu vidonda vya tumbo.

Ongeza nguvu za kiume

Fanya hivi nguvu zako za kiume.