Maumivu ya nyayo
MAUMIVU MAKALI YA NYAYO NA KISIGINO (PLANTAR FASCIITIS/POLICEMAN HEELS); UGONJWA UNAOWALIZA WATU WENGI WAKATI WA ASUBUHI.
Na Dr jimmy 0754821457.
Maumivu makali ya nyayo na kisigino(Plantar fasciitis /policeman heels) ni tatizo linalotokana na kuwepo kwa maambukizi yanayojumuisha kuvimba kwa bendi nene ya tishu ambayo hupatikana katika nyayo zetu miguuni,ambayo ndiyo inaunganisha mfupa wa kisigino na vidole vya miguu yetu (Plantar fascias).
Maambukizi katika bendi nene ya tishu zinazopatikana miguuni ambayo inaunganisha mfupa wa kisigino na vidole vya miguu yetu husababisha maumivu makali ya nyayo na kisigino(Plantar fasciitis).
maumivu makali ambayo mara nyingi hutokea asubuhi pale muhusika anapoamka na anapoweka miguu yake chini na kuanza kupiga hatua zake za kwanza asubuhi,maumivu huwa makali sana ambayo hupungua kadri anavyopiga hatua lakini pia hali ya maumivu huweza kurudi baada ya muda mrefu wa kusimama au unaposimama baada ya kukaa.
maumivu makali ya nyayo na kisigino (Plantar fasciitis) huweza kuwapata watu wa rika zote ingawa hutokea zaidi kwa watu wanaofanya mazoezi ya kukimbia sana kadhalika watu ambao ni wenye uzito mkubwa sana na wale ambao huvaa viatu visivyo na visigino na wale wanaovaa viatu vyenye visigino virefu mara kwa mara.
CHANZO CHA MAUMIVU MAKALI YA NYAYO NA KISIGINO
Inakadiriwa kuwa wanawake na wanaume walio katika umri wa miaka 40_70 wapo katika hatari kubwa ya kupata tatizo hili la maumivu makali ya nyayo na kisigino (plantar fasciitis), kadhalika wanawake wameonekana ndio wahanga wa kubwa wa tatizo hili la maumivu makali ya nyayo na kisigino ( plantar fasciitis) kuliko wanaume pia wanawake wajawazito nao wamekua wakisumbuliwa na tatizo hili vipindi vya mwisho vya ujauzito.
Mpendwa msomaji ili uweze kuelewa chanzo cha tatizo hili napenda kukujuza kua katika miguu yetu kuna tishu nyembamba ndefu inayopatikana katika maunganio ya nyayo na kisigino ambayo iko moja kwa moja chini ya miguu yetu,tishu hii inasaidia upinde wa mguu wako na kutusaidia hasa wakati tunapotembea au kusimama.
Lakini Iwapo kutatokea mvutano na msukumo mkubwa juu ya mishipa, mvutano au msukumo huo mkubwa huharibu tishu hiyo na kupelekea kupatikana maambukizi ambayo ndio chanzo cha kupata maumivu makali ya nyayo na kisigino (plantar fasciitis).
DALILI
dalili zinazoweza kukujulisha kua una ugonjwa huu wa plantar fasciitis ni kupata maumivu makali chini ya miguu yako hasa eneo la kisigino.
Mgonjwa anapoamka na anapoweka miguu yake chini na kuanza kupiga hatua zake za kwanza asubuhi hupata maumivu makali sana ambayo hupungua kadri anavyopiga hatua lakini pia hali ya maumivu huweza kurudi baada ya muda mrefu wa kusimama au unaposimama baada ya kukaa.
VIPIMO NA UCHUNGUZI
Uchunguzi wa tatizo hili kawaida hufanywa na daktari ama mtaalamu aliyebobea katika magonjwa ya mifupa hivyo baada ya kumuelezea daktari dalili zinazokusumbua daktari wako atachunguza mguu wako kwa umakini ambapo atalenga kutafuta ishara hizi:
Upinde wa juu au muelekeo wa juu ya kisigino chako
Eneo unalohisi maumivu chini ya mguu wako, iwapo ni mbele tu ya mfupa wa kisigino au la
Kuchunguza kujua maumivu makali unayapata wakati gani hasa hivyo daktari atajaribu kukupa mazoezi ili kuweza kubaini tatizo
Kadhalika daktari wako anaweza kukuagiza vipimo vifuatavyo
X_Ray na MRI_SCAN
Ili kujiridhisha kua hakuna chochote kingine kinachosababisha maumivu ya kisigino, kama vile kupasuka kwa mfupa(bone fractured)
MATIBABU YA MAUMIVU MAKALI YA NYAYO NA KISIGINO
Zipo aina kadhaa za matibabu ambazo daktari wako anaweza kukupatia ili kupunguza maumivu na kupunguza ukubwa wa tatizo.
Kadhalika Daktari Anaweza kupendekeza kutumia matibabu kadhaa kwa wakati mmoja kama ifuatavyo;
MATIBABU YA DAWA
Daktari huamua kukupatia dawa za kumeza aina ya Nonsteroidal anti inflammatory drugs (NSAIDs) kama vile ibuprofen,naproxen sodium nk.
kwaajili ya kupambana na maambukizi pamoja na kusaidia kupunguza maumivu katika kisigino.
MATIBABU YA SINDANO
Daktari huamua kukupatia matibabu ya sindano zenye steroids iwapo maumivu ni makali na matibabu ya dawa nilizoelezea hapo juu kushindwa kupunguza maumivu,
Hivyo daktari wako atakuchoma sindano ya steroid sehemu ambayo unahisi maumivu makali zaidi katika kisigino chako hii itakusaidia kupunguza maumivu kwenye kisigino kwa muda angalau wa mwezi mmoja au zaidi.
MATIBABU YA TIBA MWILI(PHYSICAL THERAPY)
Iwapo matibabu ya dawa,sindano na hata mazoezi kushindwa kusaidia kuondoa tatizo hili daktari atakupendekezea uende kwa mtaalamu wa viungo (physical therapist),Ambapo Utajifunza mazoezi ya kunyoosha na kuimarisha tishu zilizopo miguuni na misuli ya miguu ya chini. Kadhalika Mtaalam wako wa mwili anaweza pia kukupatia huduma zingine kama kukufanyia massage,kukushauri kutumia night splint,foot pads, na hata ultrasonography kusaidia kupona kwa muda mrefu.
Lakini pia Iwapo hauonyeshi maendeleo baada ya miezi kadhaa, daktari wako anaweza kupendekeza utaratibu mwingine kama vile Shockwave therapy, tenex na hata kushauri ufanyiwe upasuaji.
OPARESHENI
Daktari hufikia maamuzi ya kukufanyia upasuaji mara baada ya njia zote zilizotumika kushindwa kukusaidia yani kufanyiwa upasuaji kwa tatizo hili kawaida ni njia ya mwisho ikiwa una maumivu makali au jeraha la muda mrefu ambalo matibabu mengine hayakusaidia.
NAMNA UNAVYOWEZA KUJITIBIA NA KUPUNGUZA UKUBWA WA TATIZO LA MAUMIVU KATIKA NYAYO NA VISIGINO UKIWA NYUMBANI
Mpendwa msomaji wetu kuna njia nyingi anazoweza kuzitumia mgonjwa kujitibia au kupunguza ukubwa wa tatizo hili akiwa nyumbani lakini pia licha ya kuwa baadhi ya njia nimeziorodhesha hapa chini zimewasaidia wengi ila unahitajika kupata ushauri na vipimo kutoka kwa mtaalamu wa afya ili kujiridhisha juu ya tatizo hili kabla hujatumia njia yoyote ili akupatie ushauri ni njia gani inaweza ikakufaa bila ya kukuathiri iwapo utakua una matatizo mengine tofauti na tatizo hili.
Baadhi ya njia zinazotumika kupambana na tatizo hili ni;
1.PUNGUZA UZITO
Napenda ufahamu kwamba Mtu kua na uzito mkubwa ni miongoni mwa vyanzo vya kupata maumivu makali ya nyayo na kisigino kwani kua na uzito mkubwa huweka shinikizo au uzito zaidi kwenye tishu zilizopo miguuni. Hivyo Ikiwa una uzito mkubwa jitahidi upunguze japo kidogo ili kusaidia kupunguza shinikizo la uzito mguuni.
Unaweza kuwasiliana na daktari wako ili akupatie mpango au ratiba ya milo inayozingatia lishe bora na mazoezi ya kawaida yatakayokusaidia kupambana na tatizo hili.
2.PUMZIKA
Wakati mwingine maumivu ya nyayo na visigino ni ishara kwamba miguu yako inahitaji kupumzika tu, haswa ikiwa unafanya shughuli ngumu mara kwa mara kama vile kusimama kwa muda mrefu, kukimbia,kuvaa viatu virefu mara kwa mara hivyo basi unashauriwa kujitahidi Kujipatia mapumziko ya miguu yako kwa siku chache ili kusaidia kupunguza uvimbe na kuiruhusu tishu na misuli ya miguu kupumzika.
3.VAA VIATU VYENYE KISIGINO KIFUPI
Imeonekana kua Watu wanaovaa Viatu visivyo na visigino na viatu vyenye visigino virefu husumbuliwa sana na hili tatizo hivyo tunashauriwa kuvaa viatu vyenye visigino vifupi ambavyo vinatoa msaada mzuri kwa misuli ya miguu wakati tunapotembea au kusimama
5.INYOOSHE/KUKANDA NYAYO
wakati mwingine ili kutuliza au kupunguza maumivu yanayosababishwa na kuvimba kwa tishu, tunatakiwa kunyoosha au kujikanda na mafuta ya mzaituni kwa upole au taratibu.
Mara baada ya kumaliza shughuli zako usiku kabla hujalala paka mafuta katika nyayo zako na umuombe mkeo/rafiki/mumeo/ndugu akukande kwa muda wa dakika 15 kuanzia kwenye vidole,nyayoni akimalizia taratibu katika visigino hii husaidia hasa kuondoa maumivu na kuponya maradhi mengi na hata kuondoa uchovu wa mwili.
Health consultation
Maoni
Chapisha Maoni