Tiba ya asidi tumboni

Dr Jimmy
0620165254
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
*"ACID / TINDIKALI YA TUMBO"* - ( *GERD*  *GastroEsophagaelRefluxDesease*. )

♐Hili ni tatizo linalotokea katika mfumo wa mmeng'enyo Inayosababisha  hitilafu ya chakula au maji kurudi katika koo la chakula (umio) mara baada ya kuwa chakula Hiko kimeshamezwa.Au Ni kitendo cha kupanda kwa acids (tindikali) ya tumbo hadi kwenye Koo /Umio la chakula kwa muda mrefu na matokeo yake husababisha kiungulia (HEARTBURN)

♐Ili kuelewa vizuri tatizo hili linavyotokea tunatakiwa kujua vizuri jinsi chakula kinavyofika tumboni.

♐Kawaida Mara baada ya mtu kutafuna chakula au kunywa maji,chakula husafirishwa kupitia mrija wa chakula (Esophagus) hadi tumboni lakini juu kidogo kati ya tumbo na mrija huu wa chakula kuna kizuizi kilicho na sura ya bangili ( lower esophageal spincher )
kibangili hiki hufanya kazi ya kuzuia chakula kisurudi mdomoni au kwenye koo baada ya kuwa kimeshamezwa pia kibangiri hiki ndicho kinacho mfanya mtu aweze kula chakula huku amening'iniza kichwa chini miguu juu na chakula kisirudi tumboni.

♐Baada ya chakula kuingia tumboni huchanganyikana na vimeng'enya pamoja na tindikali ambayo hufanya kazi ya kuua vimelea vyote vilivyoingia tumboni pamoja  na chakula
mchanganyiko huu husababisha chakula kupata chachu(acids) ambayo matokeo yake huwa ni rahisi sana kuweza kurudi katika koo la chakula endapo kizuizi cha juu ya tumbo kitakua kimepata hitilafu au maambukizi.

♐KIUNGULIA (HEARTBURN)NI NIN I?♐

♐Ni hali ya kukera inayoweza kumtokea mtu yoyote na husababisha maumivu makali kwenye kifua na upande wa juu wa tumbo. 
Hali hii inaendana kwa ukaribu wa kupanda kwa tindikali(acid reflux). 

♐Lakini pia Kuna utofauti kati ya acid reflux na heartburn.

♐Kama nilivyoeleza hapo juu kuwa acid reflux ni kitendo cha kupanda kwa tindikali kutoka tumboni kurudi juu kwenye umio la chakula na kusababisha maumivu ya kifua ambayo tunaita ni kiungulia (Heartburn).

♐Kwa hiyo acid reflux ndio inayoweza kusababisha Kiungulia (HEARTBURN).

♐Hali ya kiungulia ni kitendo cha kawaida kutokea kwa watu wengi na inatokea kwa kila mtu, lakini kama tu haiambatani na maumivu makali ya kifua, kama maumivu yakizidi kuwa makali na yanatokea mara kwa mara hapo ndipo tatizo huanza.

♐Kama tatizo likiendelea zaidi basi hufikia hatua ya tatu na kuitwa gastroesophageal reflux disease (GERD), kwa hiyo kadiri kiungulia kinachukua muda mrefu mpaka kuathiri tishu za Utumbo au Umio GERD ni hatari zaidi kwa sababu inaweza kupelekea uwezekano wa kupata Madonda Tumboni au Saratani ya Koo.

♐CHANZO CHA MATATIZO♐.

♐Uchunguzi unaonyesha kuna sababu nyingi zinazoweza kuambatanishwa na matatizo haya ambayo ni;

1. Kudhohofika kwa utendaji kazi wa kizuizi cha juu ya tumbo ( Lower esophageal sphincter)

πŸ‘’Kudhohofika kwa kizuizi hiki husababishwa na utumiaji wa madawa kama nitrates , isphosphonates , Estrogen , Oral Contraceptives , Progesterone , Alpha adrenergic agents , Theophyline , Calcium channel , blockers , Benzodiazepines , Anticholinergics na tricyclic antidepressants n.k. Baadhi ya dawa zimeonekana kuharibu sana utendaji kazi wa kizuizi hiki.

 2.Mfumo dhaifu wa mmeng'enyo wa chakula :-

πŸ‘’Mfumo wa mmeng'enyo huwa dhaifu kutokana na lishe kuwa mbovu
watu wanaokula zaidi vyakula vilivyosindikwa, sukari, chocolate, vyakula vyenye caffeine kama kahawa wapo kweye hatari zaidi ya kupata matatizo haya

3.Tindikali ( Hydrochloric acid) kuzidi tumboni.

4.Upungufu wa madini kama Magnesium na Potassium

5.Uzito mkubwa na kitambi na msongo wa mawazo kupita kiasi ni chanzo cha kupata matatizo haya.

6.Wamama wajawazito na wazee wenye umri mkubwa wako kwenye hatari zaidi ya kupata matatizo haya

7.Wenye historia ya kuwa na ugonjwa wa hernia(ngiri) pia wapo katika hatari zaidi ya kupata matatizo haya

♐DALILI ZA  GASTROESOPHAGEAL REFLUX DISEASE♐

♐Dalili kuu ya matatizo haya ni kupatwa na kiungulia mara kwa mara ambapo huambatana na koo la chakula kuwaka moto pia maumivu ya kifua na hali hii huzidi zaidi pale mtu anapolala kichwa kimeinama.

♐Kiungulia hiki huanza baada ya lisaa limoja na kuisha baada ya masaa mawili baada ya kula.

♐Pia dalili za tatizo hili kwa watoto hujionesha pale mtoto anapotapika kupita kiasi au kupaliwa mara kwa mara wakati wa kula chakula.

♐Dalili zingine ni kama;

πŸ‘’Tumbo kuunguruma na Kukosa hamu ya kula chakula na kuhisi kichefuchefu.

πŸ‘’Mdomo kunuka kutokana na kurudi juu kwa chakula cha tumboni chenye tindikali.

πŸ‘’Kupata hali ya kuunguza kwenye kifua karibu na moyo, hali inayotokea Muda Mfupi  baada tu ya kula na kupata shida wakati wa kumeza chakula.

πŸ‘’ Kucheuwa Maji Maji Yenye Tindikali Ukiwa Usingizini Hasa Baada Ya Kulala Muda Mfupi Baada Ya Kula.

πŸ‘’Kukohoa au kupaliwa mara kwa mara ikiambatana na kuweweseka Kwa Kukosa Pumzi.

πŸ‘’Mdomo kuwa mchachu muda mwingi.

πŸ‘’Kupata usingizi kwa shida kutokana na maumivu ya tumbo na Koo.

πŸ‘’ Kuvimba Kwa Tezi za Shingoni Kama Vile Tonses na Goita.

πŸ‘’Mdomo kukauka.

πŸ‘’ Meno kupoteza uimara na kuanza kumomonyoka kutokana na uwepo wa tindikali.

πŸ‘’Tumbo kujaa Gesi , Kupata Choo Kama Tope Kunakoambatana kujamba sana.

πŸ‘’ Tumbo Kuunguruma Hasa Muda Mfupi Baaada Ya Kula.

♐Tatizo la Acid / Tindikali Ya Tumbo Linatibika na kupona kabisa
Health consultation
Tunajali afya yako


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi mmea huu inavyotibu vidonda vya tumbo.

Ongeza nguvu za kiume

Fanya hivi nguvu zako za kiume.