Fahamu dalili za kansa.
DALILI ZA KANSA.
Hizi ni dalili tu na sio lazima ziwe ni ugonjwa wa kansa lakini kikubwa ni kwenda hospitalini kwa vile uwezekano upo.
Hizi ni pamoja na :
1:KIKOHOZI/ MABADILIKO YA SAUTI
Kukohoa muda mrefu na pia hali hii ikaifanya sauti kuwa nzito, nyepesi au kukwaruza na hata kukwama si ya kupuuzwa.
Japo kikohozi wengi hakiwahofishi, kukohoa kwa muda mrefu na kupata makohozi yenye damu ni dhahiri jambo la kuhofiwa.
"Vikohozi vingi si kansa," anasema Therese Bartholomew Bevers, dakati na profesa wa kuzuia saratani katika taasisi ya Underson Cancer Center. "Lakini kwa hakika kukohoa makohozi yenye damu mara kwa mara kunahitaji kuchunguzwa na kuangaliwa kama kuna saratani ya mapafu inayojitokeza.
Ni lazima bingwa achunguze mapafu kwa xray au kwa CT scan kufahamu hatari ama uwezekano wa saratani unaohofiwa.
2. MATATIZO YA KUPATA CHOO
Iwapo tumbo lako litakuwa na mabadiliko kwenye utaratibu wa kupata haja usizubae tafuta tiba. Inaweza kuwa kuhara mara kwa mara, choo kupungua au kuwa na choo kidogo au kukosa haja kubwa inaweza kuwa ni tatizo kwenye utumbo mpana, anasema Bartholomew Bevers.
"Inawezekana kuna uvimbe unaozuia haja kupita kwenye utumbo na kusafiri ili kutoka nje. Huu ndiyo wakati wa kufanyiwa kipimo kinachoitwa colonoscopy kuona kama kuna uvimbe tumboni.”
3:MABADILIKO KWENYE HAJA NDOGO
"Kama kuna damu kwenye mkojo inawezekana ni saratani ya kibofu ama ya figo japo katika hali ya kawaida wengi hudhani ni tatizo la maambukizi ya njia ya mkojo UTI” Bartholomew Bevers, anaongeza.
4.MAUMIVU YA MUDA MREFU
"Si maumivu yote ni saratani lakini yale ya muda mrefu na ya mara kwa mara tena eneo moja ni lazima kuyachunguza “,Bartholomew Bevers. Mathalani ukiwa na maumivu ya mara kwa mara kichwani si kwamba una saratani ya kichwa lakini kuna jambo la kuangaliwa.
Aidha, maumivu makala kifuani pengine ni dalili ya saratani ya mapafu, pia maumivu ya mara kwa mara kwenye tumbo chini ya kitovu yaweza kuashiria saratani ya kifuko cha mayai.
5:MABADILIKO YA VIVIMBE
Kama una kivimbe au kipele usoni au popote kwenye ngozi lakini ghafla kinabadilika na kuanza kukua na kubadilika usisite kukitafutia tiba. Ni vyema kumpelekea mtaalamu wa ngozi vivimbe hivyo ili atoe maelezo na njia za tiba.
6: KIDONDA KISICHOPONA
Kama una kidonda ambacho kimekuwa na maumivu kwa wiki kadhaa nenda kwa daktari . Tunategemea miili kupona kwa muda mfupi si kwa kipindi kirefu kama wiki kadhaa, anaonya Bartholomew Bevers,
7: KUTOKWA DAMU KITATANISHI
Kwa wanawake kuona damu zinatoka nje ya mpangilio wa siku za mwezi na kwa watu wazima waliokoma hedhi ukiziona zinarudi tena usikae kimya kimbia kwa daktari. Huenda tayari umepata saratani ya shingo ya kizazi.
Lakini pia kutoka damu sehemu za haja kubwa ni dalili za saratani ya utumbo mpana, mtaalamu .
8: KUDHOOFIKA/KUPUNGUA UZITO
"Kama mtu mzima unaweza kujitahidi kupunguza uzito lakini kilo zikipungua na kukonda sana bila jitihada zozote ni suala la kupasua kichwa kuna tatizo kubwa kiafya.” Kikubwa kinachoonekana hapo ni saratani, muulize daktari.
9:KUVIMBA TEZI.
Wakati wowote unapoona una tezi au uvimbe mwilini ambao ni mgeni usiunyamazie. Inaweza kuwa ni tezi lisilo na athari ‘benign cyst’ lakini pia unaweza kuwa na saratani.
10. KUMEZA KWA TAABU..
Unaposhindwa kumeza chakula au kupata maumivu wakati ukimeza jua kuna shida kooni onana na daktari.
Uwezekano mkubwa unaweza kuwa ni kansa ya koo ama ya shingo.
"Watu wanapoona wana dalili hizo hubadili vyakula na kuanza kutumia misosi laini badala ya kuwaza kuwa ni saratani."
"Kikubwa kuanzia sasa ni hiki. Ukiona una dalili za maumivu zisizokwisha nenda hospitali na kupata uchunguzi, vipimo na matibabu usijipe majawabu ya magonjwa ambayo huyajuwi
*Ndugu zangu yapo matatizo mengi ambayo usipoyatibu Kwa haraka hupelekea kansa mfano vidonda vya tumbo,asidi tumboni,bawasiri,uvimbe kwenye kizazi,u.t.i sugu,p.i.d,fangasi n.k*
Saratani inatibika kama tiyar umeshagundulika basi njoo upate tiba ya uhakika kabisa.
Health consultation
Tunajali afya
Maoni
Chapisha Maoni