Kutokwa uchafu ukeni
𝗧𝗔𝗧𝗜𝗭𝗢 𝗟𝗔 𝗠𝗪𝗔𝗡𝗔𝗠𝗞𝗘 𝗞𝗨𝗧𝗢𝗞𝗔 𝗨𝗖𝗛𝗔𝗙𝗨 𝗨𝗞𝗘𝗡𝗜
Na Dr jimmy 0620165254
↘️Cytolytic Vaginosis Ni Nini? Mwanamke Kutoka Uchafu Mweupe Ukeni Ni Tatizo Gani?Kutoka uchafu ukeni ni moja ya matatizo yanayowasumbua sana wanawake. Uchafu huu unaweza kutoka kwa sababu nyingi, sababu zinazoonekana zaidi zikiwa ni yeast, trichomoniasis na bacterial vaginosis. Katika mada yetu ya leo tutalijadili moja la matatizo haya ambalo linasababisha mwanamke kutokwa uchafu mweupe unaoambatana na miwasho sehemu za siri ambalo kiutaalamu huitwa cytolytic vaginosis..
↘️Kimaumbile uke wa mwanamke ulio katika hali yake nzuri una aina nyingi sana za bakteria na idadi ndogo ya fungus wanaoishi ndani yake. Katika viumbe hawa wadogo wapo ambao ni rafiki na wengine ni wabaya kwa afya ya mwanamke. Bakteria rafiki hufanya kazi ya kuwadhibiti wale wabaya. Bakteria mmoja anayejulikana sana ni lactobacillus acidophilus ambaye anafanya kazi ya kuwaweka viumbe wengine pamoja na fungus kwenye idadi inayotakikana.
↘️ Cytolytic Vaginosis Husababishwa Na Nini?
Mwanasayansi Doderlein ndiye aliyegundua kuwa kiumbe ambaye anapatikana kwa wingi zaidi katika uke wa mwanamke wa umri wa kuzaa ni bakteria aitwaye lactobacillus acidophilus. Aligundua kuwa uwepo wa bakteria huyu pamoja na oestrogen ni muhimu katika kuuweka uke wa mwanamke kwenye kiwango kinachotakiwa cha pH 4.0-4.5. Lactobacilli hutengeneza tindikali (lactic acid) kutokana na glucose na kuuweka uke katika hali ya utindikali. Baada ya balehe, kwa kuwezeshwa na uwepo wa oestrogen, glycogen hutunzwa kwenye seli za ngozi laini inayotanda kuuzunguka uke, ambayo huvunjwavunjwa na seli za epithelial za uke na kuwa glucose. Lactobacilli huigeuza glucose hii kuwa lactic acid.
Baadhi ya aina za lactobacilli hutengeneza hydrogen peroxide (H2O2) ambayo ni antiseptiki (inaua baadhi ya viumbe wadogo waharibifu). Hydrogen peroxide inaweza kuzuia ukuaji wa baadhi ya wadudu wadogo kama E. coli, aina za Candida albicans, Gardnerella vaginalis na aina za Mobilincus. Inafikiriwa kuwa hydrogen peroxide inayotengenezwa na lactobacilli inaweza pia kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU). Utafiti mwingine unaonyesha kuwa lactobacilli huzuia kukua kwa candida kwa kuzuia yeast kunata kwenye seli za ngozi laini ya inayofunika uke.
Idadi ndogo ya lactobacilli (bacilli 5 kwa seli 10 za squamous) katika ute unaotoka ukeni imeonekana kuwa inasaidia kuulinda uke dhidi ya candida. Wakati mwingine bakteria hawa wa lactobacilli huongezeka sana katika mwili wa mwanamke huyu wa umri wa kuzaa. Hali hii husababisha bakteria hawa (wakati mwingine wakisaidiana na bakteria wa aina nyingine) kuharibu ngozi inayotanda uke kwa kuziua seli za ngozi hiyo wakati wakimeng’enya glycogen iliyotunzwa katika seli hizo. Cytolysis maana yake kufa kwa seli kutokana na kuharibiwa kwa ngozi laini (cell membrane) inayotanda juu ya seli hiyo.
↘️Cytolysis hutokea pale seli inaposhambuliwa na virusi, bakteria au kinga za mwili kuua seli zilizoshambuliwa na wadudu. Seli hizi zilizokufa hutoka nje ya uke na ndizo zinazosababisha uchafu mweupe, hali ambayo huitwa cytolytic vaginosis.
↘️Tatizo hili la kutoa uchafu ukeni mara nyingine husababishwa na tiba ya fungus au bakteria pale uchunguzi unapofanywa na kwa makosa kutoa tiba za antifungal au antibiotics.
↘️Wanawake wenye kisukari wanaweza kuwa na kiwango kikubwa cha glycogen (glucose kwenye maeneo ya uke) ambayo huwalisha lactobacilli na kuwafanya wazaliane kupita kiasi. Dalili huonekana zaidi wakati wa luteal (kipindi kinachoanza baada ya kutoa yai hadi siku ya kwanza ya hedhi), wakati ambapo kiwango cha oestrogen ndani ya mwili hupanda, na kusababisha kutolewa zaidi kwa glycogen na kuwalisha lactobacilli.
↘️ Dalili Za Cytolitic Vaginosis
Dalili za cytolytic vaginosis zinafanana sana na zile za yeast hivyo uchunguzi wa kina unahitajika. Kwa ujumla dalili huwa zifuatazo:
👉 . Uchafu mweupe, mwepesi au mzito
👉 . Miwasho ndani ya uke au nje (pruritus vulvae)
👉 . Maumivu hasa wakati wa kukojoa (dysuria)
👉 . Maumivu wakati wa tendo la ndoa (dyspareunia)
👉 . Uchafu kuogezeka zaidi kila mwanamke aingiapo kipindi cha luteal (baada ya kutoa yai)
👉 . Kuwa na hasira
↘️ Tiba Ya Tatizo La Kutoa Uchafu Ukeni
Bakteria hawa wa lactobacilli wanaweza kupunguzwa idadi kwa kupandisha pH ya uke kwa kutumia sodium bicarbonate (baking soda). Tiba inapaswa iwe imeweza kuurudisha uwiano wa bakteria hawa katika wiki tatu. Kama katika kipindi hicho, hali itakuwa mbaya zaidi au itabaki vile vile, acha matumizi ya baking soda na fanya uchunguzi upya.
↘️Mchanganyiko Wa Baking Soda Kwa Tiba YaCytolitic Vaginosis:
👉 . Kijiko 1-2 cha baking soda
👉 . Vikombe 4 vya maji
Jisafishe mara mbili kwa wiki, pumzika wiki moja, vivyo hivyo kwa wiki tatu.
↘️Yafuatayo yanaweza kusaidia kuongeza pH ya uke na hivyo kupunguza mwongezeko wa lactobacilli:
👉 Kupunguza au kuacha kutumia sukari
👉 Kuacha kutumia sabuni au maji ya baridi
👉 Kuacha kutumia antibiotics au dawa za fungus
👉 Kupumzika kufanya tendo la ndoa
👉 Kuacha kutumia spray za ukeni
👉 Vaa chupi za pamba na nguo zisizobana
👉 Usivae chupi usiku hii ndio shida kubwa ya wanawake wengi
👉 Kupunguza kiwango cha sukari katika mlo
↘️ Uke wa mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya vijidudu wa kuleta maradhi. Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio katika uke wa mwanamke. Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa mwili. Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha. Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eno la cervix hufanya kazi ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni. Kutoa uchafu huu sehemu za siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kitu cho chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengenezwaji wa majimaji haya ndani ya uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke.
↘️ Uchafu Wa Sehemu Za Siri Ulio Wa Kawaida
Wanawake wote hutoa uchafu sehemu za siri. Kiwango cha uchafu unaotoka, rangi yake na harufu yake vitabalikabadilika kutoka kipindi kimoja hadi kingine kulingana na muda mwanamke aliopo katika mzunguko wake wa mwezi. Uchafu huu utabadilika vilevile kama ananyonyesha, atakuwa na hisia za kufanya mapenzi, atakuwa na mabadiliko ya lishe, anatumia madawa hasa ya mpango wa uzazi au atakuwa na ujauzito. Kwa kawaida uchafu huu huwa usio na rangi, wenye rangi yenye weupe wa mawingu au njanonjano pale unapokaukia kwenye nguo. Unaweza kuwa na vijipande vidogovidogo na mara nyingine ukawa wa kunatanata.
↘️Dalili Za Uchafu Wa Ukeni Usio Wa Kawaida
Madiliko ya uwingi wa uchafu unaotoka au katika rangi ya uchafu unaotoka ni dalili ya maambukizi ya magonjwa katika uke. Maambukizi katika uke ni tatizo la kawaida kwa wanawake na wanawake wengi wameshapata tatizo la maambukizi angalau mara moja katika maisha yao. Ukiona yafuatayo, ujue unaweza kuwa na tatizo la maambukizi yavijijidudu vya maradhi katika uke wako:
👉 Kutokwa na uchafu ukeni kunakoambatana na kuwashwa au vijipele
Kutokwa na uchafu ukeni ambako ni endelevu na kwa kiwango kinachozidi kila siku
👉 Kusikia maumivu wakati wa kutoa haja ndogo
👉 Kutokwa na uchafu mweupe, mzito kama jibini
👉 Uchafu wa kijivu/mweupe au njano/kijani unaotoa harufu mbaya
↘️ Aina Za Uchafu Wa Ukeni Usio Wa Kawaida
Kitu cho chote kitakachoharibu uwiano wa bakteria wa kawaida waishio katika uke kinaweza kuleta mabadiliko katika rangi, harufu au muundo wa uchafu utakaotoka katika uke. Kwenye comments chini nitaonyesha aina ya uchafu unaotoka, maana yake au chazo chake na dalili ambazo zitatokea kwenye mwili wa mwanamke husika:
↘️ Uchafu Wenye Damu Au Wa Rangi Ya Kahawia
Hii ni dalili ya mzungumko wa mwezi wa mwanamke uliovurugika na mara chache ni dalili ya kansa ya Cervix au aina nyingine ya kansa iitwayo endometrial cancer. Mwanamke mwenye tatizo hili atatoa damu nyingi ukeni na kuumwa nyonga.
↘️Uchafu Wenye Rangi Ya Mawingu Au Njano
Hii ni dalili ya ugonjwa wa kisonono (Gonorrhea). Mwanamke atatokwa na damu katikati ya siku zake, atatokwa na mkojo bila kukusudia na kupata maumivu ya nyonga.
↘️Uchafu Wa Njano Au Kijani Wenye Harufu Mbaya
Endapo uchafu utatoka kama mapovu, wenye rangi ya kijani au njano ukiambatana na harufu mbaya , hii ni dalili ya Trichomoniasis, maambukizi (parasitic) yanayotokana na ngono zembe. Dalili nyigineni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo.
↘️Uchafu Mweupe Mzito Kama Jibini
Hii ni dalili ya maambukizi ya aina ya fungus (Yeast infection) na dalili nyingine atakazozisikia mwanamke huyu ni kuvimba na maumivu kwenye sehemu za nje za siri (vulva), kuwashwa na maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.
↘️Uchafu Mweupe, Wa Njano Au Wa Kijivu Wenye Harufu Ya Samaki
Uchafu wa aina hii ni dalili za maabukizi ya Bacterial Vaginosis. Mwanamke mwenye tatizo hili atasikia miwasho au maumivu, kuvimba kwa uke au sehemu ya nje ya uke (vulva).
↘️ Aina Ya Maambukizi Ya Ukeni
Kuifanya mada yetu iwe na maana na msaada zaidi, tutazungumzia kwa undani zaidi aina chache za maambukizi ya ukeni ambazo zinawasumbua wanawake wengi zaidi, ambapo tutatazama dalili zake na kuelezea tiba ambazo zinawea kutolewa kuondoa matatizo hayo. Hapa tutazungumzia
👉 Bacterial Vaginosis,
👉 Trichomoniasis na
👉 Monilia (Yeast) Infection.
↘️Bacterial Vaginosis:
Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakifahamiki. Kinachotokea ni kuongezeka kwa ghafla kwa idadi ya bacteria hawa ambao ni kawaida kupatikana kwenye uke na kubadilisha uwiano wao kwenye mazingira ya uke. Wanawake wenye wapenzi wengi au wanaofanya mapenzi kupitia midomo wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata maambukizi ya Bacterial Vaginosis.
↘️Dalili za Bacterial Vaginosis:
👉 Kuongezeka kwa uchafu unaotoka ukeni
👉 Kutokwa na uchafu wa kijivu/mweupe, mwepesi au wa majimaji
👉 Harufu kama ya samaki ikiambatana na uchafu
👉 Harufu inayozidi au uchafu unaozidi marabaada ya kufanya tendo la ndoa.
↘️Tiba kwa tatizo la bacterial vaginosis zipo za aina mbili. Tiba ya aina ya kwanza ni kutumia
👉 metronidazole (Flagyl),
👉 azuma au
👉 doxy na tiba ya pili ni kutumia antibiotic ya vidonge au ya cream.
↘️Trichomoniasis: Maambukizi haya hutokana na aina ya protozoa wa seli moja. Trichomoniasis maranyingi huambukizwa kwa kufanya ngono. Protozoa huyu huweza kukaa kwenye mazingira ya unyevunyevu kwa muda wa saa 24 bila kufa hivyo kufanya taulo na nguo nyingine za kuogea kuwa chanzo kingine kikuu cha maambukizi.
↘️Dalili Za Trichomoniasis
↘️ Kutokwa na uchafu wa rangi ya njano/kijani ulio kama mapovu
👉 Harufu mbaya inayoambatana na kutokwa na uchafu
👉 Kuongezeka kwa uwingi wa uchafu wa ukeni
👉 Maumivu ya ukeni au sehemu za nje ya uke (vulva)
👉 Kujisaidia haja ndogo mara nyingi zaidi
👉 Kuwashwa sehemu za siri
↘️ Tiba ya Trichomoniasis ni kunywa vidonge vya antibiotic, metronidazole, azuma, doxy
↘️ Monilia (Yeast) Infection: Kwa kawaida kuna kiwango kidogo cha yeast (Candida albicans) katik uke. Tunasema kuna maambukizi ya yeast pale kiwango chao kinapozidi hali ambayo inatokana na kubadilika kwa hali ya ukeni (change in the pH balance of the vagina). Maambukizi ya yeast hayatokani na tendo la ngono. Kuna mambo ambayo yanaweza kusababisha kuongezeka kwa yeast katika uke, nayo ni;
👉 msongo wa mawazo,
👉 matumizi ya dawa za kuzuia mimba,
👉 kisukari,
👉 ujauzito na matumizi ya antibotics.
↘️Dalili Za Monilia (Yeast) Infection
👉 Mwongezeko wa uchafu unaotoka ukeni
👉 Uchafu mweupe unaotoka katika vifungu vidogo kama vya jibini
👉 Kuwashwa na mauvivu ya ukeni au sehemu za nje (vulva)
↘️ Tiba ya Monilia (Yeast) Infection inalenga kuzuia mwongezeko wa yeast katika uke na kuwarudisha kwenye kiwango kinachofaa na si kuwaondoa. Tiba ni kutumia vidonge vya antifungal na cream za kupaka ukeni. Kuna dawa nyingi za kuweza kuondoa tatizo hili.
↘️Cytolytic Vaginosis: Hii ni hali inayojitokeza pale kunapotokea kuongezeka kwa bakteria aitwaye Lactobacillus acidophilus kwenye uke. Lactobacilli ni bakteria wazuri wanaoishi ukeni bila kuleta matatizo ya aina yo yote. Kwa kawaida uwepo wa bakteria hawa unasaidia sana katika kupambana na wadudu aina nyingine wenye madhara kwa mwili – huongeza kinga ya mwili .
Lakini endapo mazingira dhalili ya uke yatabadilika, bakteria hawa wazuri wanaweza kuzaliana kupita kiwango kinachotakiwa. Hii inaweza kutokea, kwa mfano, kunapotokea matumizi ya mara kwa mara ya antibiotics au dawa za kuzuia na kuua fungus.
Ni tatizo ambalo linawapata zaidi wanawake walio katika umri wa kuzaa – miaka 25 – 40 – kwa sababu ya uwepo wa homoni ya estrogen.
↘️Dalili za cytolytic vaginosis ni:
👉 Kutoka uchafu kwa wingi wenye rangi nyeupe, wa maji maji au mzito kama maziwa ya mgando
👉 Miwasho ya sehemu za ndani au nje ya uke
👉 Maumivu wakati wa kutoa haja ndogo
👉 Maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa
Dalili za tatizo hili ni rahisi sana kuzichanganya na zile zamatatizo mengine ya hapo juu na hasa vaginal candidiasis (monilia).
↘️Tatizo hili halina tiba bali kufanya yafuatayo:
👉 Kuacha kutumia antibiotics au dawa za fungus
👉 Kuacha kutumia sabuni ukeni na kutumia maji ya uvuguvugu tu
👉 Kutovaa nguo za ndani usiku
👉 Kutofanya tendo la ndoa
👉 Kupunguza kiwango cha sukari katika mlo
👉 Kujiosha mara kwa mara ukeni kwa kutumia baking soda. Unaweza vile vile kuchanganya baking soda na maji ukatengeneza namna ya uji na kuuweka kwenye pedi.
Soma zaidi kuhusu tatizo la cytolytic vaginosis hapo juu nimeelezea tatizo la kutoa uchafu mweupe ukeni (cytolytic vaginosis).
Katika mada yetu ya leo tumeona kwa nini uchafu hutoka katika uchi wa mwanamke, kutofautisha baina ya uchafu wa kawaida na uchafu usio wa kawaida. Tumeona vilevile aina za maambukizi ya ukeni mbayo huwasumbua wanawake wengi na tiba inayoweza kutolewa.
Tunaomba mchango wako wa mawazo kuhusu mada yetu ya leo na kama una maswali yo yote usisite kutuuliza. Ni faraja kwetu kuona tumekujibu vizuri.
*Kama Bado wasumbuka na changamoto hii na huoni pa kutokea dawa ni chai dada*
Health consultation
Maoni
Chapisha Maoni