Namna ya kuondoa gesi tumboni.
VYAKULA VYA KUONDOA GESI TUMBONI
Watu wengi walikua wakiomba mada hii japo nilishawahi kuitoa kiufupi huko nyuma. Watu wengi wamekua wakihangaika sana matumbo Yao kujaa gesi mara kwa mara na kuvimbiwa bila sababu.Leo nitaelezea jinsi ya kulitatua hili kwa kutumia vyakula na matunda, kama tatizo hili limekusumbua kwa mda mrefu, pia kuna dawa maalumu kabisa kwaajili ya tatizo hili.
Kwa njia Moja au nyingine unaweza kukuta tumbo limechafuka kwa kuuma,kujaa gesi na hata kunguruma na unaweza kuhisi unaweza kunywa dawa Ili litulie.
Katika makala niliyokuandalia Leo nimekuandalia njia Bora sana za kutuliza mchafuko wa tumbo kwakutumia vyakula na matunda badala ya dawa ambazo haziondoi chanzo Cha tatizo
JE NI NINI CHANZO?
Kabla ya kukimbilia kwenye tatizo lenyewe na matibabu ngoja tujue kwanza chanzo huanzia wapi.
Vipo vyakula na vinywaji ambavyo huchangia sana katika tatizo hili,
Vyakula na vinjwaji vinavyochangia tumbo kujaa na kukosa choo kwa mda mrefu, vinywaji ni kama;
Soda
Vilevi/pombe
Vyakula ni vyakula vyenye mafuta mengi pamoja na vyakula vyenye chumvi nyingi sana.Vyakula hivi vinapoingia tumboni huchelewa kumeng'enywa hivyo hupelekea ucheleweshaji wa usagaji wa chakula tumboni na uondoaji wa uchafu kwenye utumbo hivyo huleta kikwazo au ukinzani katika mfumo mzima wa usagaji chakula tumboni kwa urahisi.
Ili kujiepusha na matatizo ya mda mrefu na hata kuzuia uwezekano wa kuugua au magonjwa ya mara kwa mara, Huwa tunashauri kula vifuatavyo ili kusaidia usagaji mzuri wa chakula tumboni
PAPAI
Papai ni tunda ambalo Lina kimeng'enya(enzyme) ambazo husaidia usagaji mzuri wa chakula tumboni na kulifanya tumbo na utumbo kuwa laini katika usagaji wa chakula.
Watafiti wamebaini kuwa tunda hili lina harufu nzuri na ladha nzuri huboresha usagaji wa chakula,husafisha utumbo na imebainika husaidia kuondoa na kuzuia magonjwa na uvimbe tumboni na huimarisha mfumo wa Kinga mwilini.
Virutubisho vya papai pamoja na vitamin zake Zina faida nyingi sana mwilini.Papai limekuwa likitumika kama tiba tangu Karne ya 18. Kirutubisho Cha papain ambacho kipo kwenye papai ambacho kina uwezo mkubwa sana katika usagaji wa chakula tumboni, watu wengi ambao wamekuwa wakisumbuliwa na kushikwa tumbo na kupata choo kigumu Huwa wanashauriwa kutumia papai kama kilainisha tumbo.
MTINDI(YOGURT)
Mtindi ni mzuri sana katika kuondoa tatizo la gesi tumboni hata kama hupendi mtindi jitahidi kunywa kama dawa ni mzuri sana katika umeng'enyaji wa chakula tumboni. Mtindi mzuri niule ambao unatumika wenyewe bila kitu chochote. Wapo bacteria wazuri kwenye mtindi ambao husaidia sana katika uchakataji wa chakula tumboni na chakula kuwa chepesi.
UKWAJU
Kuboresha mfumo wa mmeng 'enyo na kuondoa gesi, tumia juisi ya ukwaju kurekebisha mfumo wako wa kumeng'enya chakula mwilini
Kuwa na utaratibu wakutumia vyakula hivi mara kwa mara
Kwa muendelezo ushauri na tibalishe
Maoni
Chapisha Maoni