Namna ya kupunguza kitambi
MBINU ZA KUPUNGUZA UZITO MILELE
Fanya Hivi Usiwe Miongoni Mwa Watu Watu Kati ya Wanne Wanaoongezeka Tena Baada Ya Kupunguza Uzito au Kitambi…
Kwa baadhi ya watu kupungua uzito sio kazi, wanajua mbinu zao za kufanya kupungua. Kazi ipo kwenye kufanya matokeo yawe ya kudumu.
Wengine hata hiyo kupunguza hata nusu kilo ni mtihani..
Lakini hata akipunguza baada ya muda fulani uzito unarudi kwa kasi.
Wengi wa watu kama hawa huwa wanafanya kitu kinaitwa ‘diet’
Kwa maana ya kawaida - DIET ni aina na kiasi cha chakula mtu anachokula kwa kawaida. Zingatia neno KAWAIDA!
Lakini hizo ambazo watu hufanya zinaitwa special diet..
Ambazo zinakuwa ni mpangilio aina fulani ya chakula kwa ajili ya lengo fulani maalumu au kundi fulani la watu.
Utaona kuna diet nyingi.. mfano
• Punguza kiasi unachokula. Hawa ni wale wa mchinjo. Hamu ya kula ipo hadi mbinguni lakini sasa unataka kupunguza uzito unajipakulia kiduchu au unakunywa vijuisi na mengi unaepyka kula sana
• Kuna ambao wanakuambia usijaribu kuweka mdomoni wanga au matunda matamu
• Kuna akina Dr Nanii wanakuambia kula kachumbari kabla ya kila mlo wa chakula kilichopikwa
• Wengine wanasema komaa na kiasi cha kalori unachokula. Halaf piga mazoezi ya kutosha. Hawa ni wanamhesabu wanahesabu kalori zinazoingia na zinazotoka.
Ukiweza kufanya hivi njia unaweza ukapungua tu vizuri ni kweli kila mmoja inachangamoto na faida zake zingine ni hatari kwa afya japo utapungua.
Matokeo yake yataisha siku umecha kufanya hivyo.
Kumbuka kila siku unakula kwahiyo unaongeza mafuta kwa kiasi fulani.
Ili uwe na matokeo ya kudumu yaani Permanent Weightloss lazima kitu unachokifanya kiwe na sifa zifuatazo:
1. Kiwe ni kweli limethibitika kisayansi kuwa kunasaidia watu kupungua uzito kwa muda mrefu sio kwa sababu fulani alifanya hivyo akapungua
2. Kiwe salama kiafya..
Unajua hata ukivuta sigara unapungua.. lakini je ni salama kiafya?
Diet nyingi zinakwama hapa!
Tunapotaka kupunguza uzito na kitambi pamoja na faida zingine tunatafuta kuwa na afya njema.
Kwahiyo kama hiyo diet unayofanya haikuletei afya kwa ujumla achana nayo
3. Iwe endelevu
Wanaoshindwa wengi ni kwa sababu wanadhani kupungua ni kitu cha kula chakula fulani special kama dozi ikiisha baada ya mwezi unaacha Unaendelea na mazoea yako!
Umenona kwa sababu ya ulichokula. Ili usiongezeke lazima ujenge MTINDO MPYA WA MAISHA!
Ufahamu vyakula na jinsi ya kuishi ili usiongezeke. Uifanye iwe ndio kawaida yako.
Sasa kama diet unayofanya ni gharama sana au unakula vitu ambavyo havipatikani kwenye eneo lako au ambavyo vimethibitika matokeo yake sio ya muda mrefu.. utakwama!
Hata mimi ninavyoelekeza kila kabla ya kula mchana au usiku ule kachumbari..
Hiyo ni namna rahisi yenye ufanisi sana ya kukukaribisha uanze kujifunza ‘chakula hai’
Kuna namna mamia za kuandaa chakula hai.. ni lazima ujifunze ili iwe tabia yako ya kawaida kupunguza uzito milele.
Bonyeza Link hapo chini ujifunze kwenye chaneli yangu
https://whatsapp.com/channel/0029VaDJBT8CHDyh6DLcnC0W
Maoni
Chapisha Maoni