Tambazi

Tambazi (edema) ni maradhi inayosababisha uvimbe kwenye mwili. Inaonekana hasa mkononi, mguuni na tumboni lakini inaweza kutokea pia ndani ya mwili.

Hutokea wakati viowevu (majimaji) vinatoka kwenye mishipa midogo mwilini na kukusanyika katika tishu yaani kati ya seli za mwili.

Tambazi ya mapafu (pulmonary edema) ni mkusanyiko wa majimaji kwenye mapafu. Hali hii ni hatari kwa sababu kiowevu ndani ya mapafu inaleta matata katika upumuaji, inapunguza oksijeni inayopatikana mwilini na kama ni nyingi inaweza kusababisha kifo.

Tambazi tumboni huitwa ascites.

Edema inayotokana na magonjwa ya moyo, ini na figo inatokana na kubakia kwa chumvi nyingi mno, ambayo inayatunza majimaji hayo ya ziada ndani ya mwili. Katika baadhi ya magonjwa ya ini na figo, viwango vidogo vya albumin ndani ya damu husababisha kubakia kwa majimaji. Moyo kushindwa kufanya kazi yake (heart failure), liver cirrhosis na ugonjwa wa figo uitwao nephrotic syndrome ni magonjwa yajulikanayo kusababisha edema.

Edema hutokea pale mishipa midogo ya damu iitwayo kapilari inapovujisha majimaji. Majimaji hayo hujikusanya kwenye tishu za karibu na kusababisha uvimbe.

Uvimbe usio na madhara sana husababishwa na:

. Kusimama au kukaa pahala pamoja kwa muda mrefu
. Kula chakula chenye chumvi nyingi
. Kuwa karibu na kupata hedhi
. ujauzito

Edema huweza kuwa ni matokeo ya kutumia baadhi ya madawa, kama:

. Madawa ya pressure
. Steroids
. Estrogens – madawa ya homoni
. Baadhi ya madwa ya kisukari (thiazolidinediones)

Mara nyingine, edema huwa ni ishara ya magonjwa mengine ya hatari. Baadhi ya magonjwa hayo ni:

.Congestive heart failure. Unapokuwa na tatizo hili, moja au chemba zote za chini za moyo wako zinapoteza uwezo wa kusukuma damu vizuri. Kwa jinsi hiyo, damu inaweza kurudi miguuni, kwenye ankle na nyayo na kusababisha edema. Congestive heart failure inaweza pia kusababisha uvimbe kwenye tumbo. Mara nyingine, hali hii inaweza kusababisha majimaji kujikusanya ndani ya mapafu (pulmonary edema), ambayo husababisha shida wakati wa kupumua.

.Cirrhosis. Majimji yanaweza kujaa kwenye tumbo (ascites) na miguuni kutokana na kuharibika kwa figo (cirrhosis).

.Ugonjwa wa figo. Unapokuwa na ugonjwa wa figo,majimaji ya ziada na sodium ndani ya mzunguko vinaweza kusababisha edema. Edema inayohusiana na figo mara nyingi hutokea miguuni na kuzunguka macho.

.Kuharibika kwa figo. Kuharibika kwa vijishipa vidogo vya uchuchaji katika figo huweza kusababisha nephrotic syndrome. Nephrotic syndrome ni hali ya kupungua kwa protini (albumin) katika damu kunakoweza kusababisha mkusanyiko wa majimaji na edema.

.Udhaifu au uharibifu wa veni za miguuni.

.Mfumo wa limfu usiotosheleza. Mfumo wa limfu wa mwili wako una kazi ya kukusanya  majimaji ya ziada kutoka kwenye tishu. Endapo mfumo una dosari – mathalani ukiharibiwa wakati wa upasuaji wa saratani – lymph nodes na mishipa ya limfu vinaweza kushindwa kufanya kazi vizuri na edema ikatokea.

.Upungufu mkubwa na wa muda mrefu wa protini. Upungufu mkubwa au ukosefu wa protini katika mlo wa muda mrefu unaweza kusababisha mkusanyiko wa majimaji na hivyo kupata edema.

Edema isiyo kali sana huondoka yenyewe, na hasa kama unajitahidi kukinyanyua kiungo kilichoathirika juu zaidi ya usawa wa moyo wako.

Edema kali zaidi zinaweza kutibiwa kwa kutumia madawa ambayo yanaondoa majimaji ya ziada kama mkojo (diuretics). Moja ya dawa hizi inayotumika sana ni furosemide (Lasix). Lakini daktari ndiye atakayekuamulia tiba nzuri kutokana na historia yako.

Tunaweza kuwasiliana kwa ajili ya ushauri na tiba asili.
0620165254


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi mmea huu inavyotibu vidonda vya tumbo.

Ongeza nguvu za kiume

Fanya hivi nguvu zako za kiume.