Uzazi Kwa mwanamke

KUWA DARAJA LA MKEO

Katika ya mambo yanayoongeza mvurugiko wa homoni kwa mwanamke ni MSONGO WA MAWAZO

Mwanamke akishabainika ana matatizo ya uzazi, akili yake huwa haitulii, muda wote anawaza majirani wanasemaje, ukweni wanamsema vipi, hatma ya ndoa yake ikoje kwa ufupi huwa ni kama akili yake haiko sawa, na kadri stress zinavyozidi hupelekea homoni kuendelea kuvurugika na tatizo kuzidi kuwa kubwa zaidi

Nafasi yako kama MWANAUME unaweza kumpa support SIO KIFEDHA, mpe support KISAIKOLOJIA ILI AKILI YAKE itulie aepuke msongo wa mawazo

Kuna mambo haya matano unaweza kumsaidia mkeo...

1: MPE NAFASI PALE ANAPOHITAJI NAFASI

Mwanamke mwenye matatizo ya mvurugiko wa homoni huwa ni wanawake wenye hasira za ghafla, wenye kununa, visirani, malalamiko n.k, ukigundua mkeo ana shida za namna hii usiwe mtu wa kubishana nae, mpe muda hasira yake itulie ndo muweze kuzungumza kama kuna tofauti... Ukiona haeleweki we usimsumbie jisemee kimoyomoyo kuwa naona dishi lako limeyumba kisha endelea na mambo yako ili akijituliza muongee kama marafiki

2: Mwanamke mwenye matatizo ya mvurugiko wa homoni huwa tunawapa utaratibu maalum wa vyakula, ni vizuri nawe mwanaume ukaonesha kushirikiana naye kwenye hilo... Tunawashauri wanawake kupunguza matumizi ya sukari, chipsi, nyama nyekundu n.k na kuongeza ulaji wa mbogamboga na matunda hivyo mume unaweza kuwa unamhimiza pia katika hili, sometimes ukitoka kazini mletee matunda na vile alivyoshauriwa, ukionesha kujali naye nafsi yake inatulia, kumbuka ndoa ni umoja na ushirikiano

3: ONESHA KUWA UPO NAE, hapa wanaume wengi huwa tunakwama... Usiwe busy kutafuta pesa muda wote, sometimes onesha kuwa unamjali hata huyo unayemtaftia pesa.

Muulize maswali yanayohusiana na mambo yake yake... Mfano Baby unaingia lini hedhi, hivi bado siku ngapi kuanza siku za hatari? Vipi ile dozi umefikia wapi? Onesha kwamba Afya yake ni kipaumbele kwako... Ukiskia mwanamke anahitaji attention basi ndio hiyo, kama kipindi kile cha uchumba ulivyokuwa unaulizia kama wazazi hawapo basi atoroke aje ghetto au atoroke bwenini aje ghetto au afungue shule siku moja kabla alale ghetto🀣 basi attention hiyo hiyo ioneshe kwenye ndoa...

4: MPONGEZE KWA VIJIZAWADI VIDOGO VIDOGO pale anapoonesha maendeleo mazuri kwenye afya pia kuna kale ka mbinu ka kuonesha na wewe unajifunza mambo ya afya ya mwanamke, mara mojamoja unamwambia mpenzi wangu nimekuwa nikipitia tips ya Asili Yetu Afrika nimeona kapost hiki, hebu njoo upitie au kuna daktari nimeona kaandika hivi au kasema kile hebu tujaribu na huko pia... Kadri unavyokuwa karibu na mkeo ndivyo anasahau kelele za ukweni, mawifi na marafiki, homoni zikibalansi usishangae kupata hata mapacha... 

Allah akupe hekima katika kuilinda ndoa yako

Good morning


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi mmea huu inavyotibu vidonda vya tumbo.

Ongeza nguvu za kiume

Fanya hivi nguvu zako za kiume.