Elewa juu ya rhesus factor

Kuna makundi ya damu yafuatayo A,B,AB na O

Unapopimwa kundi la damu wanaweza kubainisha kama una Rh Factor au hauna,

Rh-factor ni protein ambayo inakutwa katika baadhi ya Seli hai nyekundu za damu, na sio kila mtu anayo hii protein katika cell zake.

Waliyonayo ndo wanaitwa Positive na wasiyonayo ni negative, so ukienda hospital utaambiwa ni either A+/A- or B+/B-, AB+/AB- au O+/O-

MUHIMU: Ikitokea mama ni mjamzito na ana blood group yenye NEGATIVE, baba wa Mtoto akawa na POSITIVE,

 Mara nyingi inategemewa mtoto atakuwa na POSITIVE aliyoirithi kwa baba yake, so kinachotokea ni kwamba kwa ujauzito wa kwanza tatizo linaweza lisionekane kwasababu damu ya mama na mtoto havichanganyikani, 

Lakini wakati wa kujifungua damu inaweza kumix hivyo mwili wa mama utatambua hiyo RH-PROTEIN ambayo ipo kwa mtoto hivyo mwili wake huanza kuzalisha kinga mwili ikijua kwamba hicho ni kitu kigeni kinachotakiwa kushambuliwa

So, kwa mimba ya pili sasa mama mwili wake unakuwa tayari umetengeneza kinga mwili kwa ajili ya kupambana na RH positive yoyote itakayoingia hivyo cells za mtoto zitashambuliwa na kingamwili za mama kama hatua sitahiki hazitachukuliwa

HATUA STAHIKI: Mama kama ni negative na baba ni positive, ujauzito unapofikisha week ya 28 Mama anatakiwa kuchoma chanjo ya kuzuia uzalishaji wa kingamwili za kushambulia Cells za mtoto iitwayo ANT-D na ya pili ni ndani ya masaa 72 baada ya mama kujifungua,

Kama mama una high risk pregnancy au unajua kabisa una hili group la damu lenye negative na baba ni positive jitahidi sana uanze clinic mapema mnoooooo

NB:KAMA BABA NA MAMA NI NEGATIVE WOTE HAINA SHIDA BUT MPIME KUWA NA UHAKIKA ZAIDI NDO MAANA CLINIC YA KWANZA BABA ANASISITIZWA KUWEPO

Kuna watu ambao huwa hawajui hili swala hasa vijijini unashangaa mama anajifungua mtoto wa kwanza vizuri wanaofatia wote anakuwa anawapoteza, hii inaweza kuwa moja ya sababu. 

Kama Makala Hii Imekusaidia, Sio Vibaya Ukishea kwa Wengine Nao Wajifunze


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi mmea huu inavyotibu vidonda vya tumbo.

Ongeza nguvu za kiume

Fanya hivi nguvu zako za kiume.